Exodus 35:4-9

Vifaa Kwa Ajili Ya Maskani Ya Mungu

(Kutoka 25:1-9)

4 aMose akaiambia jumuiya yote ya Waisraeli, “Hili ndilo Bwana aliloamuru: 5 bToeni sadaka kwa Bwana kutoka mali mliyo nayo. Kila mmoja aliye na moyo wa kupenda atamletea Bwana sadaka ya dhahabu, fedha na shaba; 6nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, za rangi nyekundu na kitani safi; singa za mbuzi; 7ngozi za kondoo dume zilizopakwa rangi nyekundu, na ngozi za pomboo;
Pomboo hapa ina maana ya mnyama mwenye ngozi laini aishiye kwenye milima yenye misitu, au pengine nguva au sili.
mbao za mshita;
8 dmafuta ya zeituni kwa ajili ya taa; vikolezi kwa ajili ya mafuta ya upako, pamoja na uvumba wa harufu nzuri; 9vito vya shohamu, na vito vingine vya thamani vya kuweka kwenye kisibau na kile kifuko cha kifuani.

Copyright information for SwhNEN